Shirika la Habari la Hawza- Kufuatia shinikizo kubwa la kisiasa na kijamii kutoka kwenye taasisi za kiraia, Uhispania imefuta kwa upande mmoja mkataba wa uuzaji wa silaha kwa kampuni ya Kizayuni ya IMI.
Mkataba huu, ambao ulikuwa na thamani ya takriban euro milioni 6.8 (sawa na dola milioni 7.8) kwa ajili ya ununuzi wa risasi na silaha kwa Jeshi la Walinzi la Raia wa Uhispania, ulifutwa baada ya maandamano ya mara kwa mara yaliyofanywa na wananchi pamoja na baadhi ya maafisa, maandamano ambayo yalitokana na wasiwasi mkubwa kuhusiana vita ya kikatili ya Israel dhidi ya watu wanyonge wa Ghaza.
Aidha, serikali ya Uhispania siku ya Alhamisi ilitangaza kuwa mazungumzo ya pande mbili ya kufuta mkataba huo yameshindika, na kwa kuwa upande wa Israel ulikataa, Uhispania ililazimika kuufuta kwa upande mmoja.
Mwanzoni, habari za mkataba huu ziliposambaa katika anga ya kisiasa na kijamii ya Uhispania, vuguvugu la maandamano lililipuka na kufanya hali ya nchi kuwa tete, kwa sababu mkataba huo ulikuwa na ukeukwaji wa wazi wa sheria iliyopitishwa hapo awali nchini Uhispania inayopiga marufuku biashara na Israel wakati wa vita vya Ghaza.
Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sánchez, pamoja na Yolanda Díaz na wizara husika, baada ya juhudi nyingi za kutafuta kufutwa kwa mkataba huo kwa njia ya makubaliano ya pande mbili, walilazimika hatimaye kuufuta kwa upande mmoja kutoka upande wa Hispania.
Vita vinavyo fanywa na Israel dhidi ya Ghaza hadi sasa vimesababisha kuuawa kwa zaidi ya watu 51,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Takwimu hizi za kutisha zimezifanya nchi mbalimbali, ikiwemo Uhispania, kutathmini kwa umakini zaidi uhusiano wao wa kijeshi na wa kidiplomasia pamoja na "Israel."
Maoni yako